Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
AUTHOR:๐ป๐โ๐ผโ๐๐โ13
JINSI YA KUPIKA KABABU ZA NYAMA YA KUSAGA
♦️MAHITAJI
๐ Nyama ya kusaga Kilo 1
๐ Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa Kijiko 1 cha chai
๐ Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko 1 cha chai
๐ Bizari ya Kababu ½ paketi
๐ Chumvi kiasi
๐ Mafuta kiasi ya kukaangia
๐ Mayai 2
๐ slice za mkate 2
♦️JINSI YA KUPIKA
1. Weka nyama Yako katika bakuli kubwa
2. loweka slice za mkate katika maji kisha zikamue maji uzivuruge kwa mkono ndani ya nyama hakikisha zinachanganyika na nyama vizuri
3. Changanya nyama pamoja na viungo vyote katika bakuli.
4. Chukuwa mayai yako vunjia katika huo mchanganyiko changanya tena mpaka vichanganyike
5. Fanya madonge shape ya duara kama kwenye picha weka kando.
6. Kisha Kaanga kama sambusa mpaka Zibadilike rangi.
7. Epua zikiwa tayari kwa kuliwa.
FINISH
๐๐โ๐ธโ๐๐๐ผ๐ธ ๐๐ธ๐๐ธโ๐พ๐ธโค๐ ๐น๐ผ๐ โ๐ 15000 ๐๐ ๐๐๐ธ ๐๐๐๐ 3 ๐๐ธ๐๐ ๐๐ธ๐๐๐๐๐ธโ๐ธ โ๐ธ๐๐ ๐๐๐ธ 0752338972
๐๐๐๐๐๐ 5๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐
๐๐-๐
๐
(๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐)
1:NI PORTABLE (MAHALI POPOTE UNAWEZA UKATEMBEA NAYO
2:INA POWER BANK KWAAJILI YAKUTUNZIA CHAJI PINDI UMEME UMEKATIKA
3:INAUWEZO MKUBWA WA KU CONNECT VIFAA64 (SIMU,COMPYUTER) NA BADO IKAWA NAKASI YA HALI YA JUU
4: AIRTEL ROUTER INA UWEZO WAKUSHIKA HADI MITA MIA
N.B HAINA KIKOMO MWEZI MZIMA
NIWEWE TU
๐๐๐๐๐๐/๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐
๐๐๐๐๐๐
● 110,000 ina mbs..... 30
● 150,000 ina mbs 50
● 200,000 ina mbs 100
AGIZA NASI ☎️0782657014
๐LOCATION: DAR-ES-SALAAM .....MBEZI BEACH..
Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
LAMBALAMBA ZA MAZIWA
๐๐ MAHITAJI.....
1.Sukari kiasi Chako
2.Rangi yoyote
3.Maziwa fresh nusu lita
4.Vanilla ya Maji au unga kifuniko 1
5.Vikopo vya lamba lamba
6.vijiti vya lamba lamba
7:Custard powder kikombe kimoja CHA robo
๐๐JINSI YA KUANDAA÷ANZA KUCHEMSHA MAZIWA YAKO KWA MOTO MDOGO TU WA KAWAIDA HAKIKISHA YASI SHIKE CHINI
๐งKISHA WEKA UNGA WA CUSTARD KOROGA HADI UWONE MAZIWA YAMEANZA KULETA UZITO YATOE JIKON
๐งKISHA YATIE MAZIWA YAKO KWENYE MAJI YA LITA 5 .
๐งBAADA YA HAPO CHANGANYA SUKARI HADI IWE TAMU KISHA WEKA RANGI YEYOTE RANGI WEKA KIDOGO SANA TIA VANILLA KISHA TAYARISHA VIKOPO.UKISHA MIMINA
๐ง MCHANGANYIKO WAKO KATIKA VIKOPO ANZA KUWEKA VIJITI (PIA UNAWEZA KUTUMIA MAZIWA YA UNGA VIJIKO 3-4 VYA CHAKULA KADRI UNAVYO HITAJI UZITO WA LAMBA LAMBA.
Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
JINSI YA KUTENGENEZA UROJO
- Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbali mbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja
- Hapa nitaeleza jinsi ya kuupika huo uji(urojo) mpaka kukamilika kwake
- Asili ya urojo ni India ila kwa sasa nchi mbali mbali zina andaa upishi huu
- Na Zanzibar ni mlo unaopendwa na maarufu sana
KWENYE UROJO TUNAWEKA VITU VIFUATAVYO
1- Mbatata za Kuchemsha
2- Mayai Ya Kuchemsha
3.Bagia za dengu
4- Bagia kunde
5- Chatne
6- Chipsi Za Muhogo
7- Mishkaki
8- Kachori
9- Katlesi
10- Na urojo wenyewe Urojo Sauce
11- Pilipili ya kupika
12- Majani ya spinach
13- Majani ya gilgilani
JINSI YA KUANDAA UJI WA UROJO
MAHITAJI
1- Viazi mviringo/mbatata – kg1
2- Unga wa ngano – 1/2kg
3- Binzari (rangi ya mchuzi) – kijiko kimoja
4- Malimao au ndimu – 4
5- Chumvi kiasi
6- Maji ya kutosha kulingana na mahitaji
7- Mbogamboga
8- Giligilani
MANDAALIZI
- Safisha viazi mbatata/ mviringo bila kumenya kisha vichemshe
- Chemsha hivyo hivyo bila kumenya hakikisha havivurugiki vikiiva ipua na uviweke pembeni
- Bandika sufuria lingine la maji huku pembeni ukikoroga unga wa ngano uliochanganywa na maji (uji wa ngano) kwenye bakuli, endelea kukoroga unga wa ngano mpaka uwe mwepesi na usiwe na madonge, kisha weka binzari
- Maji ya jikoni yakishachemka, mimina mchanganyiko wako wa ngano na binzari kwenye maji ya moto koroga uji wako hadi ushike vizuri uji ukisha shika vizuri kamulia malimao na punguza moto na uuache uji uendelee kuchemka, wakati uji ukiendelea kuchemka menya vile viazi vyako ulivyo vichemsha mwanzo na uvikate vipande saizi ya kati kisha vimimine (tumbukiza) katika uji uliopo jikoni
- Acha mchanganyiko wako uchemke kwa dakika tano kisha ipua urojo wako utakuwa tayari kwa Biashara
- Unaweza kuchanganya urojo wako na kachori, bagia, mishikaki, crips za viazi au mihogo iliyo katwa katwa vipande vidogo vidogo
- Pia unaweza weka mboga mboga (figiri, majani ya kitunguu majani ya kabichi na tayari kwa kuliwa.
enjoy๐๐๐
BIRIANI YA KUKU WA KIENYEJI
MAHITAJI ๐
BASMAT RICE
RANGI ZA CHAKULA
TOMATO PASTE
NYAMA YA KUKU
NYANYA MAJI
MAZIWA MTINDI
VITUNGUU MAJI
CHUMVI
MAFUTA YA KUPIKIA
VIAZI MVIRINGO
GILIGILANI
ZABIBU KAVU
Kitunguu saumu na tangawizi
Carrot
Hoho
Binzari ya manjano
Binzari nyembamba
Namna ya kutayarisha ๐ค
Chukua nyama yako ya kuku ioshe ichemshe weka Kitunguu saumu tangawizi ,limao na iache ichemke mpaka iive
Baada ya kuiva Chukua nyanya maji katakata weka kwenye blender pamoja na GILIGILANI na maziwa mtindi saga kwa pamoja
Chukua Sufuria Weka mafuta ya kutosha Kisha Chukua Vitunguu maji ulivyokata vya kutosha kaanga vikiwa Golden brown vitoe weka kwenye sahani
Kwenye mafuta yaleyale kaanga viazi mviringo vyako na vikiwa brown vitoe
Chukua Sufuria Weka ile nyama ya kuku na weka ule mchanganyiko wa nyanya na mtindi Vitunguu maji ,mafuta ya kupikia ,Chumvi ,Kitunguu saumu na tangawizi na mafuta kiasi acha vichemkie
Vikichemka weka tomato paste, binzari ya manjano na binzari nyembamba changanya Kisha weka Hoho na carrot acha vichemkie Kisha Weka viazi mviringo acha mchuzu uchemke mpka uwe mzito
Chukua Sufuria Weka maji kiasi yakichemka weka Chumvi mafuta ya kupikia na mchele wako koroga kidogo kidogo mpka maji yakauke
Yakikauka Chukua rangi zako kulingana na rangi unazopenda mwagia kwa juu na utatupia zabibu kavu Kisha palilia wali wako au funika kwa mfuko laini baada ya hapo utageuza na utachanganya na rangi zako uchanganyikane vizuri pakua chakula chako rosti la nyama weka kwa juu na biriani lako lipo tayari kuliwa na pilipili
Enjoy ๐๐๐๐๐๐
Jifunze kupika mapishi hapa mapishiclub.Blogspot.Com
Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .
Vipimo
Unga 1 ½ vikombe vya chai
Mafuta ¼ kikombe cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Maji 1 kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Mayai 6 mayai
Manda nyembamba za mraba
(Spring roll pastries sheet) 6
Nyama ya kusaga ½ kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe
Chumvi kiasi
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi kiasi (ukipenda)
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike
Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.
Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.
Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .
Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.
Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.
Weka kwenye sahani tayari kuliwa.
Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA
orodha ya viungo
Mchele kilo1 ¼
Nyama kilo ½
Mafuta yakupikia lita ¼
Njegere kilo ½
Giligilani pakti ndogo 1
Mdalasini ya unga packti ndogo 2
Jira packti ndogo 2
Chumvi packti ndogo 1
Vitunguu-maji kubwa 3
Vitunguu-saumu kubwa 1
Hatua ya kutayarisha viungo
Ukisha andaa vitu vyote hivi tunaanza kuandaa chakula chetu cha Leo
Anza kumenya vitunguu saumu
Katakata vitunguu maji
Chambua girigilan
Kata kata nyama
Chukua vitunguu swaumu, girigilan, jira viweke kwenye kiuri na utwange vizuri hadi vilainike
Hatua na maelekezo ya kupika
Chukua sufuria yako bandika jikoni weka mafuta
Weka vitunguu maji jikoni
Kaanga hadi viwe na ranging ya kahawia
Weka nyama anza kuikaanga
Endelea kugeuza nyama yako ikaange vizuri hadi iive
Chukua mchanganyiko wa vitunguu swaumu, girigilan, jira ulio twanga viweke na endelea kukaanga
Chukua mdalasin weka koroga vizuri
Weka chumvi geuza
Weka njegere zako geuza vizuri ichanganyike
Weka maji acha ichemke kwa dakika tano
Weka mchele geuza vizuri taraaraatibu
Funika na uweka moto mdogo wakuivisha chakula taratibu kwa dakika kumi
Funua chakula chako geuza hapo kitakua pilau iliyo tayari kwa kula
Hitimisho na Mawasiliano ya Mwandishi
Kwa kuhitimisha napenda kusema tu kwamba upishi wa pilau uko wa aina nyingi na hata ndani ya aina moja bado mapishi yanaweza kutofautiana sana na inategemea Zaidi ubunifu wa mpisha kuweza kupindisha pindisha baadhi ya taratibu ili kuweza kupata chakula kizuri, kitamu na kinacho walaji.
Mfano tu kwenye pilau ya nyama unaweza weka nyama nyingi, kawaida au chache, unaweza kubadilisha rangi ikawa kahawia au njano nk
je una maoni usisite kituandikia jjumbe yako katika ukurasa wetu
by Director13
Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
Kupunguza uzito kunaweza kuhusisha mabadiliko kadhaa ya mtindo wa maisha. Hapa kuna mambo machache unayoweza kufanya:
1. **Lishe Bora:** Punguza ulaji wa kalori na uzingatie vyakula vyenye lishe kama matunda, mboga za majani, protini za nyama ya kuku au samaki, na nafaka nzima.
2. **Mazoezi:** Fanya mazoezi mara kwa mara, angalau dakika 30 kila siku. Hii inaweza kuwa kutembea, kukimbia, au mazoezi mengine yanayokufurahisha.
3. **Kunywa Maji:** Kunywa maji ya kutosha kila siku. Maji husaidia katika mmeng'enyo wa chakula na kuzuia kiu ambayo inaweza kuchangia kula zaidi.
4. **Kupunguza Mlo wa Haraka:** Epuka vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi, na vyakula vilivyosindikwa.
5. **Lala Vya Kutosha:** Uhakikishe unapata usingizi wa kutosha kila usiku. Kulala vya kutosha kunaweza kusaidia kudhibiti hamu ya kula na kuboresha ustawi wako kwa ujumla.https://www.highcpmgate.com/zx2v4eizi?key=aa435f5c317faedefcc8f4c2186b880f
Kumbuka kwamba kila mtu ni tofauti, na mchakato wa kupunguza uzito unaweza kuhitaji uvumilivu na muda. Ni vizuri kushauriana na daktari au mtaalamu wa lishe kabla ya kuanza mpango wowote wa kupunguza uzito ili kuhakikisha unafuata njia inayofaa kwako.
KATLESI / katles
mahitaji
-viazi mbatata - ½
-Nyama ya kusaga robo
-Mayai 3
-Vitunguu maji Vikubwa 2
-pilipili hoho 1
-karoti 1
-Ndimu / limau
-Pilipili manga - kijiko cha chai ½
-Tangawizi mbichi
-Kitunguu thomu
-Bizari ya mchuzi kijiko cha chai 1
-chumvi kiasi
-Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani -kikombe 1cha mafuta ya kupikia
namna ya kupika:
-Menya viazi vikate na uchemshe vikiwa vinakaribia kuiva weka binzari ya manjano, ndimu na chumvi, vitunguu maji, hoho na karoti(iliyokwanguliwa) kisha utaviponda kwa pamoja mpka viwe kama ugali.
-Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, pilipilimanga mpaka ikauke.
- Sasa changanya vizuri na viazi ulivyoviponda ponda na nyama uliyoitia viungo, changanya vizuri mpaka viazi vichanganyike vizuri na nyama.
-Sasa fanya madonge na uviringe kama shepu ya yai au duara kawaida.
-Sasa vunja yale mayai kisha uyakoroge kwenye kibakuli pembeni, baada ya chukua vile viazi vyenye shepu ya duara uvigaragaze kwenye chenga za mkate, vyote viwe vimepakwa chenga za mkate; kisha utachovya kwenye ute wa yai na kuzichoma kwenye mafuta mpaka ziwe na rangi ya dhahabu.
baada ya hapo tayari kuliwa.
NB:- unaweza kutumia nyama ya kuku, au samaki bila kusahau kutoa miba.
-kama hauna chenga za mkate unaweza kutumia unga wa ngano uliochanganywa na sembe kidogo.
-Epuka kugeuza geuza ili zisije zikavurugika kwenye mafuta, na mafuta yawe yamepata moto kiasi kwani zikikaa sana jikoni pia zinaweza kuvurugika.
BISKUTI ZA SIAGI
Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30
MAHITAJI
➖Kikombe 1 siagi
1/2 kikombe icing sugar
➖Kijiko 1 cha chai vanilla extract
➖Vikombe 2 unga wa ngano
1/4 kijiko cha chai chumvi
MAELEZO
⭕Anza kwa kuwasha oven joto la 175 degrees C ili ipate joto wakati unachanganya unga. Kwenye bakuli kubwa changanya siagi, icing sugar na chumvi mpaka mchanganyiko ulainike vizuri. (unaweza kutumia mashine au bila mashine. Ni rahisi zaidi ukitumia mashine). Ongeza vanilla, changanya kwa dakika kama moja nyingine
⭕Ongeza unga wa ngano. Kanda mpaka uchanganyike vizuri kabisa
⭕Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha kijiko 1 cha chakula, tengeneza mduara kama vimpira. Panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea.
⭕Hakikisha umeacha nafasi ya kutosha katikati ya kila biskuti.
⭕Kandamiza kila donge la biskuti kwa kutumia cookies stamp, uma, glasi ya maji au kifaa chochote utakachotumia kutengeneza umbo unalotaka
⭕Hakikisha unachovya kifaa cha kutengenezea umbo la biskuti kwenye icing sugar ili kusaidia unga usinate kwenye kifaa na pia umbo litokee vizuri zaidi
⭕Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 175 degrees kwa dakika 12-15 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini.
⭕ Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida
⭕Ipua, acha zipoe kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa.
Kwa mapishi zaidi ya cookies na biscuits, jipatie kitabu