π™‹π™„π™‡π˜Όπ™ π™‰π™”π˜Όπ™ˆπ˜Ό π™‹π™„π™Žπ™ƒπ™„ π™‡π˜Όπ™†π™€

Welcome mapishiclub.Blogspot.Com JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA orodha ya viungo Mchele kilo1 ¼ Nyama kilo ½ Mafuta yakupikia lita ¼ Njegere kilo ½ Giligilani pakti ndogo 1 Mdalasini ya unga packti ndogo 2 Jira packti ndogo 2 Chumvi packti ndogo 1 Vitunguu-maji kubwa 3 Vitunguu-saumu kubwa 1 Hatua ya kutayarisha viungo Ukisha andaa vitu vyote hivi tunaanza kuandaa chakula chetu cha Leo Anza kumenya vitunguu saumu Katakata vitunguu maji Chambua girigilan Kata kata nyama Chukua vitunguu swaumu, girigilan, jira viweke kwenye kiuri na utwange vizuri hadi vilainike Hatua na maelekezo ya kupika Chukua sufuria yako bandika jikoni weka mafuta Weka vitunguu maji jikoni Kaanga hadi viwe na ranging ya kahawia Weka nyama anza kuikaanga Endelea kugeuza nyama yako ikaange vizuri hadi iive Chukua mchanganyiko wa vitunguu swaumu, girigilan, jira ulio twanga viweke na endelea kukaanga Chukua mdalasin weka koroga vizuri Weka chumvi geuza Weka njegere zako geuza vizuri ichanganyike Weka maji acha ichemke kwa dakika tano Weka mchele geuza vizuri taraaraatibu Funika na uweka moto mdogo wakuivisha chakula taratibu kwa dakika kumi Funua chakula chako geuza hapo kitakua pilau iliyo tayari kwa kula Hitimisho na Mawasiliano ya Mwandishi Kwa kuhitimisha napenda kusema tu kwamba upishi wa pilau uko wa aina nyingi na hata ndani ya aina moja bado mapishi yanaweza kutofautiana sana na inategemea Zaidi ubunifu wa mpisha kuweza kupindisha pindisha baadhi ya taratibu ili kuweza kupata chakula kizuri, kitamu na kinacho walaji. Mfano tu kwenye pilau ya nyama unaweza weka nyama nyingi, kawaida au chache, unaweza kubadilisha rangi ikawa kahawia au njano nk je una maoni usisite kituandikia jjumbe yako katika ukurasa wetu by Director13

Post a Comment

0 Comments