Chapati za nyama

Welcome mapishiclub.Blogspot.Com MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA . Vipimo Unga 1 ½ vikombe vya chai Mafuta ¼ kikombe cha chai Chumvi ½ kijiko cha chai Maji 1 kikombe cha chai Mafuta ½ kikombe cha chai Mayai 6 mayai Manda nyembamba za mraba (Spring roll pastries sheet) 6 Nyama ya kusaga ½ kilo Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe Chumvi kiasi Pilipili manga ½ kijiko cha chai Pilipili mbichi kiasi (ukipenda) Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai. Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1. Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe. Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba . Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha. Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi. Weka kwenye sahani tayari kuliwa.

Post a Comment

0 Comments