Biriani la kuku wakienyeji

BIRIANI YA KUKU WA KIENYEJI MAHITAJI 😚 BASMAT RICE RANGI ZA CHAKULA TOMATO PASTE NYAMA YA KUKU NYANYA MAJI MAZIWA MTINDI VITUNGUU MAJI CHUMVI MAFUTA YA KUPIKIA VIAZI MVIRINGO GILIGILANI ZABIBU KAVU Kitunguu saumu na tangawizi Carrot Hoho Binzari ya manjano Binzari nyembamba Namna ya kutayarisha 🖤 Chukua nyama yako ya kuku ioshe ichemshe weka Kitunguu saumu tangawizi ,limao na iache ichemke mpaka iive Baada ya kuiva Chukua nyanya maji katakata weka kwenye blender pamoja na GILIGILANI na maziwa mtindi saga kwa pamoja Chukua Sufuria Weka mafuta ya kutosha Kisha Chukua Vitunguu maji ulivyokata vya kutosha kaanga vikiwa Golden brown vitoe weka kwenye sahani Kwenye mafuta yaleyale kaanga viazi mviringo vyako na vikiwa brown vitoe Chukua Sufuria Weka ile nyama ya kuku na weka ule mchanganyiko wa nyanya na mtindi Vitunguu maji ,mafuta ya kupikia ,Chumvi ,Kitunguu saumu na tangawizi na mafuta kiasi acha vichemkie Vikichemka weka tomato paste, binzari ya manjano na binzari nyembamba changanya Kisha weka Hoho na carrot acha vichemkie Kisha Weka viazi mviringo acha mchuzu uchemke mpka uwe mzito Chukua Sufuria Weka maji kiasi yakichemka weka Chumvi mafuta ya kupikia na mchele wako koroga kidogo kidogo mpka maji yakauke Yakikauka Chukua rangi zako kulingana na rangi unazopenda mwagia kwa juu na utatupia zabibu kavu Kisha palilia wali wako au funika kwa mfuko laini baada ya hapo utageuza na utachanganya na rangi zako uchanganyikane vizuri pakua chakula chako rosti la nyama weka kwa juu na biriani lako lipo tayari kuliwa na pilipili Enjoy 😋😋😋😋😋😋 Jifunze kupika mapishi hapa mapishiclub.Blogspot.Com

Post a Comment

0 Comments