Upishi wa urojo wa pemba

Welcome mapishiclub.Blogspot.Com JINSI YA KUTENGENEZA UROJO - Urojo ni mchanganyiko wa vyakula mbali mbali pamoja na uji uji wake katika bakuli moja - Hapa nitaeleza jinsi ya kuupika huo uji(urojo) mpaka kukamilika kwake - Asili ya urojo ni India ila kwa sasa nchi mbali mbali zina andaa upishi huu - Na Zanzibar ni mlo unaopendwa na maarufu sana KWENYE UROJO TUNAWEKA VITU VIFUATAVYO 1- Mbatata za Kuchemsha 2- Mayai Ya Kuchemsha 3.Bagia za dengu 4- Bagia kunde 5- Chatne 6- Chipsi Za Muhogo 7- Mishkaki 8- Kachori 9- Katlesi 10- Na urojo wenyewe Urojo Sauce 11- Pilipili ya kupika 12- Majani ya spinach 13- Majani ya gilgilani JINSI YA KUANDAA UJI WA UROJO MAHITAJI 1- Viazi mviringo/mbatata – kg1 2- Unga wa ngano – 1/2kg 3- Binzari (rangi ya mchuzi) – kijiko kimoja 4- Malimao au ndimu – 4 5- Chumvi kiasi 6- Maji ya kutosha kulingana na mahitaji 7- Mbogamboga 8- Giligilani MANDAALIZI - Safisha viazi mbatata/ mviringo bila kumenya kisha vichemshe - Chemsha hivyo hivyo bila kumenya hakikisha havivurugiki vikiiva ipua na uviweke pembeni - Bandika sufuria lingine la maji huku pembeni ukikoroga unga wa ngano uliochanganywa na maji (uji wa ngano) kwenye bakuli, endelea kukoroga unga wa ngano mpaka uwe mwepesi na usiwe na madonge, kisha weka binzari - Maji ya jikoni yakishachemka, mimina mchanganyiko wako wa ngano na binzari kwenye maji ya moto koroga uji wako hadi ushike vizuri uji ukisha shika vizuri kamulia malimao na punguza moto na uuache uji uendelee kuchemka, wakati uji ukiendelea kuchemka menya vile viazi vyako ulivyo vichemsha mwanzo na uvikate vipande saizi ya kati kisha vimimine (tumbukiza) katika uji uliopo jikoni - Acha mchanganyiko wako uchemke kwa dakika tano kisha ipua urojo wako utakuwa tayari kwa Biashara - Unaweza kuchanganya urojo wako na kachori, bagia, mishikaki, crips za viazi au mihogo iliyo katwa katwa vipande vidogo vidogo - Pia unaweza weka mboga mboga (figiri, majani ya kitunguu majani ya kabichi na tayari kwa kuliwa. enjoy🙃🙃😃

Post a Comment

0 Comments