𝙅𝙞𝙛𝙪𝙣𝙯𝙚 𝙠𝙪𝙩𝙚𝙣𝙜𝙚𝙣𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙖𝙩𝙡𝙚𝙨𝙞

KATLESI / katles mahitaji -viazi mbatata - ½ -Nyama ya kusaga robo -Mayai 3 -Vitunguu maji Vikubwa 2 -pilipili hoho 1 -karoti 1 -Ndimu / limau -Pilipili manga - kijiko cha chai ½ -Tangawizi mbichi -Kitunguu thomu -Bizari ya mchuzi kijiko cha chai 1 -chumvi kiasi -Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani -kikombe 1cha mafuta ya kupikia namna ya kupika: -Menya viazi vikate na uchemshe vikiwa vinakaribia kuiva weka binzari ya manjano, ndimu na chumvi, vitunguu maji, hoho na karoti(iliyokwanguliwa) kisha utaviponda kwa pamoja mpka viwe kama ugali. -Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, pilipilimanga mpaka ikauke. - Sasa changanya vizuri na viazi ulivyoviponda ponda na nyama uliyoitia viungo, changanya vizuri mpaka viazi vichanganyike vizuri na nyama. -Sasa fanya madonge na uviringe kama shepu ya yai au duara kawaida. -Sasa vunja yale mayai kisha uyakoroge kwenye kibakuli pembeni, baada ya chukua vile viazi vyenye shepu ya duara uvigaragaze kwenye chenga za mkate, vyote viwe vimepakwa chenga za mkate; kisha utachovya kwenye ute wa yai na kuzichoma kwenye mafuta mpaka ziwe na rangi ya dhahabu. baada ya hapo tayari kuliwa. NB:- unaweza kutumia nyama ya kuku, au samaki bila kusahau kutoa miba. -kama hauna chenga za mkate unaweza kutumia unga wa ngano uliochanganywa na sembe kidogo. -Epuka kugeuza geuza ili zisije zikavurugika kwenye mafuta, na mafuta yawe yamepata moto kiasi kwani zikikaa sana jikoni pia zinaweza kuvurugika.

Post a Comment

0 Comments