KATLESI / katles
mahitaji
-viazi mbatata - ½
-Nyama ya kusaga robo
-Mayai 3
-Vitunguu maji Vikubwa 2
-pilipili hoho 1
-karoti 1
-Ndimu / limau
-Pilipili manga - kijiko cha chai ½
-Tangawizi mbichi
-Kitunguu thomu
-Bizari ya mchuzi kijiko cha chai 1
-chumvi kiasi
-Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani -kikombe 1cha mafuta ya kupikia
namna ya kupika:
-Menya viazi vikate na uchemshe vikiwa vinakaribia kuiva weka binzari ya manjano, ndimu na chumvi, vitunguu maji, hoho na karoti(iliyokwanguliwa) kisha utaviponda kwa pamoja mpka viwe kama ugali.
-Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, pilipilimanga mpaka ikauke.
- Sasa changanya vizuri na viazi ulivyoviponda ponda na nyama uliyoitia viungo, changanya vizuri mpaka viazi vichanganyike vizuri na nyama.
-Sasa fanya madonge na uviringe kama shepu ya yai au duara kawaida.
-Sasa vunja yale mayai kisha uyakoroge kwenye kibakuli pembeni, baada ya chukua vile viazi vyenye shepu ya duara uvigaragaze kwenye chenga za mkate, vyote viwe vimepakwa chenga za mkate; kisha utachovya kwenye ute wa yai na kuzichoma kwenye mafuta mpaka ziwe na rangi ya dhahabu.
baada ya hapo tayari kuliwa.
NB:- unaweza kutumia nyama ya kuku, au samaki bila kusahau kutoa miba.
-kama hauna chenga za mkate unaweza kutumia unga wa ngano uliochanganywa na sembe kidogo.
-Epuka kugeuza geuza ili zisije zikavurugika kwenye mafuta, na mafuta yawe yamepata moto kiasi kwani zikikaa sana jikoni pia zinaweza kuvurugika.
Showing posts with label MAPISHI. Show all posts
Showing posts with label MAPISHI. Show all posts
BISKUTI ZA SIAGI
Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30
MAHITAJI
➖Kikombe 1 siagi
1/2 kikombe icing sugar
➖Kijiko 1 cha chai vanilla extract
➖Vikombe 2 unga wa ngano
1/4 kijiko cha chai chumvi
MAELEZO
⭕Anza kwa kuwasha oven joto la 175 degrees C ili ipate joto wakati unachanganya unga. Kwenye bakuli kubwa changanya siagi, icing sugar na chumvi mpaka mchanganyiko ulainike vizuri. (unaweza kutumia mashine au bila mashine. Ni rahisi zaidi ukitumia mashine). Ongeza vanilla, changanya kwa dakika kama moja nyingine
⭕Ongeza unga wa ngano. Kanda mpaka uchanganyike vizuri kabisa
⭕Gawanya mchanganyiko wa unga kwa kipimo cha kijiko 1 cha chakula, tengeneza mduara kama vimpira. Panga vizuri kwenye chombo cha kuokea ukitumia karatasi za kuokea.
⭕Hakikisha umeacha nafasi ya kutosha katikati ya kila biskuti.
⭕Kandamiza kila donge la biskuti kwa kutumia cookies stamp, uma, glasi ya maji au kifaa chochote utakachotumia kutengeneza umbo unalotaka
⭕Hakikisha unachovya kifaa cha kutengenezea umbo la biskuti kwenye icing sugar ili kusaidia unga usinate kwenye kifaa na pia umbo litokee vizuri zaidi
⭕Oka kwenye oven iliyopata moto katika joto ya 175 degrees kwa dakika 12-15 au mpaka zianze kupata rangi ya kahawia chini.
⭕ Usishangae zikiwa laini sana wakati unazitoa kwenye oven, ni kawaida zikipoa zinakuwa kawaida
⭕Ipua, acha zipoe kwa dakika 5 kabla ya kuhamishia kwenye waya wa kupozea zipoe kabisa.
Kwa mapishi zaidi ya cookies na biscuits, jipatie kitabu
MKATE WA MAYAI ( SPONGE CAKE )
*MAHITAJI*
 Mayai sita
 Sukari nusu kikombe
unga kikombe kimoja
hiliki
 vanilla(si lazima)
zabibu kavu(si lazima)
baking powder kijiko cha chai 1
*MATAYARISHO*
Tayarisha sufuria ya kiasi na uipake mafuta.
Weka mayai, sukari na iliki kwenye bakuli uanze kupiga Kwa mashini(mixer) au mchapio mpaka mayai yafure yaani yazidi yawe mara mbili yake.
Anza kuweka unga kidogo kidogo huku ukikoroga taratibu kisha ufuatie na vanilla.
Weka mchanganyiko wote kwenye sufuria.
Tupia tupia zabibu juu ya mchanganyiko.
Bake mkate wako Kwa moto wa juu na chini kwenye jiko la makaa( hakikisha moto kwenye jiko ni kidogo sana alafu ukifinika ueke makaa ya kutosha juu ya utakachofunikia sufuria, mfuniko
 unaweza ukabake kwa oven kwa Moto wa 250°C takriban nusu saa(itategemea na aina ya oven)
bofya mkate wako Kwa kijiti. Kijiti kikitoka kikavu mkate upo tayari.
NB:
zingatia:
*mkate wa mayai hautiwi siagi, blueband, butter wala mafuta.
Ni ngano tu na mayai
*kipimo kizuri cha mkate cha mayai ni ujazo wa ngano na ujazo wa mayai uwe sawa sawa, yaani kwa mfano unga glass moja basi na mayai yafikie ujazo huo huo wa glass moja.
*wakati wa kupiga mayai inatakiwa usiache ache mkono, upige au kukoroga mpaka yafanye povu; itafanya mkate uvimbe vizuri.
*mkate huu uko soft na mlaini kuliko keki ndio maana ukaitwa sponge cake.
MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .
Vipimo
Unga 1 ½ vikombe vya chai
Mafuta ¼ kikombe cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Maji 1 kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Mayai 6 mayai
Manda nyembamba za mraba
(Spring roll pastries sheet) 6
Nyama ya kusaga ½ kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe
Chumvi kiasi
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Pilipili mbichi kiasi (ukipenda)
Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike
Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.
Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.
Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .
Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.
Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.
Weka kwenye sahani tayari kuliwa.
📌 BIRIANI
MAHITAJI
▪Nyama - kilo moja na nusu
▪Mchele kilo moja wa basmat
▪Chumvi - kiasi
▪Mafuta - 1 Kikombe
▪Samli - ½ Kikombe
▪Kitunguu(Kata virefu virefu) - 3Vikubwa
▪Nyanya (kata vipande) - 2
▪Nyanya kopo - 1 Kijiko cha chakula
▪Kitunguu saumu 1 Kijiko cha chakula
▪Tangawazi - 1 Kijiko cha chakula
▪Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
▪Pilipili ya unga nyekundu - ½ Kijiko cha chai
▪Majani ya kotmiri iliyokatwa - 2 Vijiko vya chakula
▪Viazi 10
▪Gram masala - 1 Kijiko cha chai
▪Mtindi - robo Kikombe cha chai
JINSI YA KUPIKA
1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitunguu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama robo kikombe, acha moto mdogo mdogo kama robo saa, epua weka pembeni.
VPIMO VYA WALI WA BIRIANI.
▪Mchele - Vikombe 5 vikubwa (Kikombe cha chai)
▪Hiliki nzima - 4
▪Mdalasini mzima - 1
▪Rangi ya biriani - robo Kijiko cha(yoyote upendayo)
▪Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu - nusu Kikombe
▪Chumvi - kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA WALI WA BIRIANI
1.Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
2. Chemsha maji kwenye sufuria Vikombe 10
3. Tia hiliki na mdalasini kwenye maji.
Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
Unamimina tena ule mchele nusu kwenye sufuria, unatia rangi kidogo, halafu unamimina
mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia. Kisha chukua
mafuta unamimina juu ya mchele, unarudisha jikono unaweka
moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
byee