📌 BIRIANI
MAHITAJI
▪Nyama - kilo moja na nusu
▪Mchele kilo moja wa basmat
▪Chumvi - kiasi
▪Mafuta - 1 Kikombe
▪Samli - ½ Kikombe
▪Kitunguu(Kata virefu virefu) - 3Vikubwa
▪Nyanya (kata vipande) - 2
▪Nyanya kopo - 1 Kijiko cha chakula
▪Kitunguu saumu 1 Kijiko cha chakula
▪Tangawazi - 1 Kijiko cha chakula
▪Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
▪Pilipili ya unga nyekundu - ½ Kijiko cha chai
▪Majani ya kotmiri iliyokatwa - 2 Vijiko vya chakula
▪Viazi 10
▪Gram masala - 1 Kijiko cha chai
▪Mtindi - robo Kikombe cha chai
JINSI YA KUPIKA
1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitunguu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama robo kikombe, acha moto mdogo mdogo kama robo saa, epua weka pembeni.
VPIMO VYA WALI WA BIRIANI.
▪Mchele - Vikombe 5 vikubwa (Kikombe cha chai)
▪Hiliki nzima - 4
▪Mdalasini mzima - 1
▪Rangi ya biriani - robo Kijiko cha(yoyote upendayo)
▪Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu - nusu Kikombe
▪Chumvi - kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA WALI WA BIRIANI
1.Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
2. Chemsha maji kwenye sufuria Vikombe 10
3. Tia hiliki na mdalasini kwenye maji.
Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
Unamimina tena ule mchele nusu kwenye sufuria, unatia rangi kidogo, halafu unamimina
mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia. Kisha chukua
mafuta unamimina juu ya mchele, unarudisha jikono unaweka
moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
byee
0 Comments: