Mapishi ya vikokoto vitamu

MAPISHI YA VIKOKOTO VITAMU

NOTE: mapishi haya yaliyoandaliwa na director kessy sio kwa ajili ya vitafunio tu unaweza ukafunguwa biashara au ukasambaza madukani baada ya kutengeneza na ukajipatia kipato

. MAHITAJI YAKE

Unga – Vikombe 2

. .

Samli – 2 Vijiko vya chakula

. .

Maziwa ¾ Kikombe

. .

Iliki – Kiasi

. .

Mafuta ya kukarangia Kiasi

. .

MAHITAJI YA :SHIRA

Sukari – 1 Kikombe

. .

Maji ¾ Kikombe

. .

Vanila ½ Kijiko cha chai

JINSI YA KUPIKA

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya. Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.

Halafu fanya viduara vidogo vidogo, sukuma kwenye kibao ,meza kisha kata shape utakayopenda wew. Kisha kahanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi , kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.

Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa. ✍️DIRECTOR KESSY

Post a Comment

0 Comments