*PISHI LA MKATE WA SINIA AU KUMIMINA*
*Mahitaji*
```🥥mchele wa mikate nusu na robo
🥥nazi za size tatu kama kubwa mbili
🥥sukari nyeupe robo
🥥hamira 1 tsblespoon
🥥hiliki 1 tablespoon
🥥samli au mafuta
Roweka mchele wako usiku kucha au masaa 6 mpaka 8.
Saga nazi zako upate tui zito ujazo wa lita moja,
Kwenye jagi la blenda
Weka mchele wako, tui, hamira na hiliki
Sagaa mpaka vilainike kusiwe na chenga za mchele.
Ukishasagika vizuri weka kwenye bakuli funika uumuke.
Wakati unaumusha, koleza jiko lako la mkaa likolee haswa
Uji wako wa mkate ukishaumuka vizuri
Weka sukari koroga mpaka kusiwe na mapovu..
Hapa jiko lako tayari lishashika vizuri moto, punguza moto kwenye jiko jengine, ilo liloshika moto libaki na moto wa kiasi sio mwingi ili usiunguze mkate maana na jiko lenyewe tayari lishashika moto,,kwenye jiko la pili ongezea na makaa ili moto usife ili tuje kuufunikia mkate wetu kwa juu.
Kisha weka sufuria ya kupikia mkate jikoni ipate moto,weka na samli kijiko kimoja au mafuta vijiko viwili yakisha pata moto,mimina mkorogo wako wa mchele funika kwa sinia lako lisilo na moto juu,hapa utakaa kias dakika 10 kisha utakuwa ushakazana mkate kwa chini ,sasa utaweka moto juu usiwe mkali sanaaa ukaunguza mkate,,weka moto wa kuivisha na kupigisha rangi,,,usikae mbali ukaunguza pishi lako.
Utakaa kias dakika 10 hivi funua angalia ukianza kupiga rangi na unaushika kama umekazana hauhisi uji uji katkat bas utauangalia kama tayari utaepua.
Ukishaepua ufunike usiuwache wazi ukakamaa juu..funika ile kile jasho la mkate unafanya kuwa mlaini...kama utakuwa na haraka na mkate wako basi chukua chombo kikubwa kama beseni weka maji kisha weka sufuria yenye mkate ufunike usiuwache wazi ili upoe kwa haraka.
Ukishapoa utautoa uukate```
0 Comments
Welcome to comment