Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
*JINSI YA KUPIKA DONATI YA HAMILA NA SUKARI YA KUGANDA* .
*Vipimo*
```Unga mweupe 2 ½ Vikombe vikubwa (mugs)
Siagi 2 vijiko vya supu
Hamira 2 vijiko vya chai
Yai 2
Mtindi 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga 2 vijiko vya supu
Maji 1 ¼ takriban
Mafuta ya kukaangia
*Namna Ya Kutayarisha Na Kupika* Ikiwa hamira ni ya kuumua haraka (instant yeast) weka vitu vyote pamoja katika bakuli uchanganye vizuri uwe uzito wake kama wa mkate wa ufuta na sio mlaini sana kama wa kaimati.
Funika uumuke mchanganyiko kisha teka vidonge uchome katika mafuta makali kiasi.
3-Epua zichuje mafuta kisha mwagia sukari uliyokwishatayarisha iliyokwishapoa.
Shira ya kuganda
Sukari 2 gilasi
Maji ½ gilasi
Hiliki ½ kijiko cha chai
Weka katika sufuria, weka katika moto mdogo mdogo ichemke huku unakoroga usiachie mkono.
Endelea kukoroga mpaka ifanye povu na inate.
Epua ipowe umimine katika donuts uchanganye changanye mpaka shira igeuke sukari nyeupe ya kuganda (glazed)
Vidokezo:
Unaweza kutia nazi ya chenga
Unaweza kutia shira aina nyenginezo kama caramel, shira ya kawaida, maziwa mazito (condensed) au shira ya tende.```
0 Comments
Welcome to comment