Welcome mapishiclub.Blogspot.Com
JINSI YA KUPIKA NDIZI ZA NYAMA YA NG'OMBE.
Picha By Chef Victoria Mgaya
Mahitaji Ya Jinsi Ya Kupika Ndizi Za Nyama
1. Ndizi mbichi 10-20
2. Nyama ng’ombe 1 kilo moja
3. Kitunguu maji 2
4. Nyanya 2
5. Kitunguu saumu 7
6. Tangawizi 1 kipande
7. Ndimu 2
8. Chumvi kiasi
9. Mafuta kiasi
Jinsi Ya Kupika Ndizi Za Nyama
1. Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi.
2. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive.
3. Menya ndizi ukatekate.
4. Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia Nyanya uendelea kukaanga.
5. Tia tangawizi na thomu ilobakia.
6. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake.
7. Ziache ndizi ziive mpaka zikiwa tayari
Kujiunga Na group Letu Bonyeza Hapa 👉 mapishiclub.blogspot
0 Comments
Welcome to comment