create by Director13
JINSI YA KUPIKA KARANGA ZA MAYAI
Mahitaji Ya Kupika Karanga Za Mayai
1. Karanga kilo moja.
2. Mayai 2
3. Chumvi kijiko kimoja.
4. Sukari kiasi unachohitaji.
5. Unga wa ngano robo kilo
6. Mafuta ya kupikia.
Jinsi Ya Kupika Karanga
1. Chukua karanga weka katika sinia,chambua kuondoa karanga mbovu,na taka taka.
2. Baada ya kuchambua weka katika bakuli au chombo cha kukandia,piga mayai katika chombo pembeni na uweke chumvi. Tia mayai katika karanga na kisha zichanganye kuhakikisha zote zimekolea mayai.
3. Chukua kiasi cha sukari unachokadiria
kitakufaa.Tia katika ule mchanganyiko wa
karanga,mayai na chumvi kisha
4. Changanya ili sukari inate katika karanga
zote.
5. Chukua unga tia katika mchanganyiko wako, changanya vizuri kuhakikisha karanga
zote zimekuwa nyeupe kwakufunikwa na unga.
6. Weka mafuta kiasi kwenye kikaango, yakichemka anza kukaanga karanga zako
hakikisha unazitoa kabla hazijawa brown sana usijeunguza karanga zako.
#MTAG RAFIKI YAKO AJE AJIFUNZE MAPISHI
Usisahu kuLIKE na KuComment
💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝💝❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥❤️🔥
Director13 created
0 Comments: